Friday, 1 April 2016

MBUNGE WA MANONGA AMETOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO

Mashindano ya UMISETA NA UMITASHUMITA nchini yakitazamiwa kuanza  hivi karibuni kitaifa, kiwilaya na kimkoa, Mbunge wa jimbo la Manonga (Igunga Tabora) Seif Khamis Gulamali, ametoa vifaa vya michezo katika shule za sekondari na shule za msingi katika jimbo lake
Pichani; Wa kwanza kulia Mbunge wa Manonga Seif Khamis Gulamali akiwa katika pozi na
moja ya wachezaji wa timu ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania (Picha na Maktaba)

Mbunge huyo ametoa vifaahivyo vya michezo katika Shule 13 za Sekondari na Shule za Msingi karibu 50 za Jimbo la Manonga.
"Kwa kuanzia Tumezipatia Vifaa vya Michezo kama Mipira ya Footballs, Netballs, Basketballs, Handballs na Volleyballs,"Jumla ya Mipira 180 tumegawa nikiwa kama Mbunge wa Jimbo la Manonga ikiwa na lengo la kukuza na kuboresha sekta ya Michezo Jimboni". Amesema Mh. Seif Khamis Gulamali
Mh Gulamali amesema hii itapelekea kukuza Viwango vya wanamichezo katika jimbo la Manonga na wilaya ya Igunga kwa ujumla ndio maana ametoa vifaa hivyo

0 comments:

Post a Comment