MANCHESTER UNITED YAFANYA MAAJABU OLD TRAFFORD JANA DHIDI YA OLYMPIACOS
Timu ya soka ya huko England Manchester united imeweza kufanya maajabu baada ya kuichabanga goli tatu kwa besen timu ya Olympiacos katika mechi yao ya marudiano iliyofanyika hapo jana katika viwanja vya OLD TRAFFORD nchini Uingereza....Ikikaririwa kuwa Manchester united ilipigwa goli mbili kwa sufuri na timu hiyo ya Olympiacos katika mechi yao ya mwanzo ya ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA mnamo wiki mbili zilizopita...
Mechi ya jana ilikuwa kati ya mechi tatu ambazo zinakiweka kibarua cha kocha mkuu wa timu hiyo mzee David Moyes ila ikawauzuri baada ya timu hiyo kushinda.....
![]() |
KOCHA WA MANCHESTER UNITED DAVID MOYES |
![]() |
KIKOSI CHA TIMU YA MANCHESTER UNITED |
Mpaka kufikia dakika tisini za mchezo Man u ilikuwa ikiongoza kwa mabao matatu kwa mtungi na kujiwekea nafasi hukoo kwwenye nane bora ikiungana na timu za Chelsea,Real madrid na zinginezo.
0 comments:
Post a Comment