
Vyombo vya habari vya Serikali ya
Syria vimesema jeshi limemuua kamanda wa kijeshi kutoka kundi la waasi
lenye uhusiano na Al Qaeda, la Nusra Front.
Nusra front ni moja kati ya makundi yenye nguvu yanayopambana ili kumuangusha Rais wa Syria, Bashar Al Assad, kundi hilo pia lilihusika na shambulizi mjini Aleppo.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria ameweka wazi nia yake ya kufanya mazungumzo na Nusra Front ikiwa sehemu ya jitihada za kurejesha utulivu mjini Aleppo.