Tuesday, 26 August 2014

MABINGWA MARA MBILI MFULULIZO WA KOMBE LA TASWA WAPIGWA MVUA YA MABAO LEO



MABINGWA MARA MBILI MFULULIZO WA KOMBE LA      TASWA WAPIGWA MVUA YA MABAO LEO

Mabingwa wa kombe la taswa kanda ya kaskazini ambao ni chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) wamemiminiwa mvua ya magoli matatu kwa mbili na timu ya SOMBETINI PARISH FC mapema leo.

 Mtanange huo ambao umepigwa mida ya saa kumi za jioni katika viwanja vya FFU Arusha umezikutanisha timu hizo mbili katika robo fainali ya kombe la NANI ZAIDI lililojumuisha timu kama AJtC stars,Sombetini Parish fc,FFU na zingine kibao.
Ikiwa na mchezo wa sita kwa kila timu Sombetini Parish imejiwekea rekodi ya kutofungwa mechi hata moja katika ligi hii wakiwa wameibuka na ushindi wa michezo mitatu na suluhu katika michezo mitatu waliyoweza kucheza.

Na timu ya Ajtc stars imeweza kushinda michezo mitatu,sare mchezo mmoja  na kuchabangwa katika michezo miwili waliyoweza kucheza katika ligi hii,matokeo yamchezo wa leo umeitoa timu ya Ajtc stars katika mashindano na kuiruhusu Sombetini parish kuingia katika nusu fainali ya ligi hii.
Mabao katika mchezo huo,Ajtc stars ilianza kwa kutupia goli kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na mshambuliaji wa timu hiyo Fred ’16 dakika ya tatu ya mchezo huo ambae pia alirudi golini na kutupia bao la pili katika dakika ya tisini ya mchezo.

Pichani ni baadhi ya wachezaji wa Ajtc stars
 Kwa upande wa washindi wa mchezo huo Sombetini Parish  mabao yaliwekwa kimyani na Emmanuel ’11 katika dakika arobaini ya mchezo,bao la pili kupitia nahodha wa timu hiyo Sam Petro dakika arobaini na tano ya mchezo na kapu la  mabao lilihitimishwa na Frank Ally kupitia mkwaju wa penati dakika ya sabini ya mchezo.

(Pichani) Kocha wa AJTC stars bwana Idrissa Bakari akiongea na wanahabari uwanjani Field force leo



 Mchezo huo ambao timu hizo zilionyesha kukamiana na kila mmoja kutaka kulichungulia lango la mwenzie ila Sombetini iliibuka kidedea kwa mabao 3-2 dhidi ya Ajtc stars.
Akizungumza na IGUNGA NEWS kocha wa timu ya Ajtc stars amesema huo ni moja ya mchezo sababu kuna kushinda,kushindwa na suluhu na kupoteza mchezo wa leo ni changamoto kwake,Pia akaongezea kusema japo watu wanamlaumu kuchezesha mamluki katika kikosi chake akasema hayo ni maneno ya mashabiki tu. 

           “unajua kushindwa,kushinda na suluhu ni moja ya mchezo na kupoteza mchezo wa leo ni changamoto kwangu na siwezi kuwa ‘’BLAME’’ wachezaji wangu wameshindwa kutengeneza ‘’chemistry’’ ya mchezo na nahitajika kujipanga kwa michuano mingine kuhusu mamluki hao ni mashabiki tu wanaongea hivyo”,alisema kocha Idrissa Bakari

Pichani Mwenye suti nyeusi Kocha wa Sombetini bwana Kamanda akitoa ufafanuzi juu ya mchezo wa leo kwa waandishi wa habari leo
Nae kocha wa Sombetini Parish amesema ushindi huu ulikuwa ni wa lazima kwao kutokana na maandalizi ya michuano hiyo waliyoyafanya kuanzia mwanzo na wamejipanga vizuri katika kuingia katika nusu fainali ya michuano hiyo na amelaumu kwa wachezaji wake kupewa kadi zisizo za lazima.

         ‘’Yaa ushindi wa leo ulikua ni wa lazima kwetukutokana na maandalizi katika mashindano haya tuliyoyafanya tokea mwanzo na tumejipanga vizuri kwa kufanya mazoezi na leo tumepewa kadi zisizo za lazima ila si kwamba timu haina nidhamu’’,alisema kocha Kamanda.

Pichani mashabiki wa Sombetini Parish wakisherehekea ushindi dhidi ya Ajtc stars
 Ushindi wa leo umewapa nafasi Sombetini Parish kuwa na mchezo siku ya ijumaa na wanasema wamejipanga vyema katika kuingia kwenye mchezo huo na kuahidi ushindi kwa timu hiyo.
Pia IGUNGA NEWS iliweza kuongea na mashabiki wa timu zote mbili na kusema timu zo zimecheza vilivyo na matokeo yaliyotokea ni moja ya mchezo na wameahidi kuendelea kuzishabikia timu zao.  

Friday, 15 August 2014

 Taarifa Ya Wizara Ya Afya Kuhusu Ugonjwa Wa Ebola Kuingia Tanzania Zijue Na Dalili Zake {2014}

Wahudumu wa afya wakimsaidia mgonjwa wa ebola

Ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa vya habari na kuihusisha Tanzania.
Pichani;Baadhi ya wahudumu wa afya

 Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo

Waziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa.

 Kupitia ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII 

Mnamo mwezi wa Machi 2014 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi ambao ulianzia katika ya Guinea na kusambaa katika nchi za Siera Leone, Liberia na Nigeria. Hadi tarehe 31 Julai, 2014 idadi ya wagonjwa ilikuwa 1323 na vifo 729.

 Ugonjwa wa Ebola husababishwa na virusi vya Ebola. Dalili zake ni homa kali ya ghafla, kulegea mwili, maumivu ya misuli, kuuma kichwa, na vidonda kooni. 

Mara nyingi dalili hizo hufuatiwa na kutapika, kuharisha, vipele vya ngozi, figo na ini kushindwa kufanya kazi na kwa baadhi ya wagonjwa kutokwa damu ndani na nje mwilini. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi. 

Ugonjwa wa Ebola unaambukiza kwa kasi na unaenea kati ya mtu na mtu kwa: o kugusa damu na majimaji kutoka mwilini mwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo o kugusa maiti wakati ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huu. 

 kugusa wanyama walioambukizwa Mizoga na wazima kama vile sokwe na swala wa msitu. 

Aidha Ugonjwa wa Ebola hauna tiba wala chanjo. Hadi sasa hapa nchini Tanzania hakuna mgonjwa yoyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa virusi vya Ebola.

 Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii imeandaa mikakati ya kuzuia ugojnwa huu usiingie hapa nchini na ikiwa utaiingia uweze kudhibitiwa kabla haujasambaa. 

Mikakati hiyo ni pamoja na:  Kuunda kikosi kazi (Task Force) kinachohusisha wajumbe mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo ikiwa ni pamoja na WHO, UNICEF, USAID na CDC kwa ajili ya kuweka mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu ikwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa mpango wa dharura wa kukabiliana na Ebola ambao tayari umeandaliwa. 

 Kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Makatibu Tawala na Waganga Wakuu wote wa Mikoa. 

Aidha taarifa hii pia imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Fact sheet” ya ugonjwa, Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli, na na namna ya kuwahudumia wagonjwa. 

 Kuboresha ufuatiliaji na utambuzi wa ugonjwa katika maeneo ya viwanja vya ndege na mipakani ili kuweza kubaini wasafiri watakaoonyesha dalili za ugonjwa au wenye viashiria hatari. . 

Miongozo ya utoaji elimu imeandaliwa ikiwemo Vipeperushi. Aidha watalaamu wa Afya wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili endapo ugonjwa huo ukitokea uweze kutolewa taarifa mapema 

 Vifaa kinga (Personal Protective Gears) vipo vya kutosha na Wizara imeanza kuvisambaza kutoka bohari za kanda za MSD na kuzipeleka kwenye vituo vya kutoa huduma za afya ili watumishi wa afya waweze kutumia iwapo mgonjwa atajitokeza. 

Aidha idadi itaongezwa kadiri ya mahitaji yatakavyojitokeza. 
 Wizara imebainisha vituo vya kutolea huduma kwa mikoa yote iwapo endapo ugonjwa huu utatokea hapa nchini. Aidha katika vituo hivi, vifaa kinga pamoja na madawa vimeshaandaliwa. 

Kuwasiliana na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa maendeleo ili kuweza kupata msaada wa mahitaji mbalimbali kama yalivyoainishwa kwenye mpango wa dharura wa kukabliana na Ebola ulioandaliwa. 
Hitimisho Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu ila kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu. 

Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika. Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu ni:- o Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola 
 Wananchi wanatahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa akiwa na dalili za Ebola; badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri. 

 Wananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola. o Zingatia usafi wa mwili tabia na kiroho. 

 Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa Serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola. 
 Kuwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu. 
Wizara itaendelea kushirikiana na sekta mbalimbali kuimarisha ufuatiliaji ili kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini. KUMBUKA KU SHARE NA WATANZANIA WENZAKO

thanx to www.jimmcartertz.com