MABINGWA
MARA MBILI MFULULIZO WA KOMBE LA TASWA
WAPIGWA MVUA YA MABAO LEO
Mabingwa wa kombe la taswa kanda ya kaskazini ambao
ni chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) wamemiminiwa mvua ya
magoli matatu kwa mbili na timu ya SOMBETINI PARISH FC mapema leo.
Mtanange huo ambao umepigwa mida ya saa kumi za
jioni katika viwanja vya FFU Arusha umezikutanisha timu hizo mbili katika robo
fainali ya kombe la NANI ZAIDI lililojumuisha timu kama AJtC stars,Sombetini
Parish fc,FFU na zingine kibao.
Ikiwa na mchezo wa sita kwa kila timu Sombetini
Parish imejiwekea rekodi ya kutofungwa mechi hata moja katika ligi hii wakiwa
wameibuka na ushindi wa michezo mitatu na suluhu katika michezo mitatu
waliyoweza kucheza.
Na timu ya Ajtc stars imeweza kushinda michezo
mitatu,sare mchezo mmoja na kuchabangwa
katika michezo miwili waliyoweza kucheza katika ligi hii,matokeo yamchezo wa
leo umeitoa timu ya Ajtc stars katika mashindano na kuiruhusu Sombetini parish
kuingia katika nusu fainali ya ligi hii.
Mabao katika mchezo huo,Ajtc stars ilianza kwa
kutupia goli kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na mshambuliaji wa timu hiyo
Fred ’16 dakika ya tatu ya mchezo huo ambae pia alirudi golini na kutupia bao
la pili katika dakika ya tisini ya mchezo.
 |
Pichani ni baadhi ya wachezaji wa Ajtc stars |
Kwa upande wa washindi wa mchezo huo Sombetini
Parish mabao yaliwekwa kimyani na Emmanuel
’11 katika dakika arobaini ya mchezo,bao la pili kupitia nahodha wa timu hiyo
Sam Petro dakika arobaini na tano ya mchezo na kapu la mabao lilihitimishwa na Frank Ally kupitia mkwaju
wa penati dakika ya sabini ya mchezo.
 |
(Pichani) Kocha wa AJTC stars bwana Idrissa Bakari akiongea na wanahabari uwanjani Field force leo |
|
|
|
Mchezo huo ambao timu hizo zilionyesha kukamiana na
kila mmoja kutaka kulichungulia lango la mwenzie ila Sombetini iliibuka kidedea
kwa mabao 3-2 dhidi ya Ajtc stars.
Akizungumza na IGUNGA NEWS kocha wa timu ya Ajtc
stars amesema huo ni moja ya mchezo sababu kuna kushinda,kushindwa na suluhu na
kupoteza mchezo wa leo ni changamoto kwake,Pia akaongezea kusema japo watu
wanamlaumu kuchezesha mamluki katika kikosi chake akasema hayo ni maneno ya
mashabiki tu.
“unajua kushindwa,kushinda na suluhu ni
moja ya mchezo na kupoteza mchezo wa leo ni changamoto kwangu na siwezi kuwa
‘’BLAME’’ wachezaji wangu wameshindwa kutengeneza ‘’chemistry’’ ya mchezo na
nahitajika kujipanga kwa michuano mingine kuhusu mamluki hao ni mashabiki tu
wanaongea hivyo”,alisema kocha Idrissa Bakari
 |
Pichani Mwenye suti nyeusi Kocha wa Sombetini bwana Kamanda akitoa ufafanuzi juu ya mchezo wa leo kwa waandishi wa habari leo |
Nae kocha wa Sombetini Parish amesema ushindi huu
ulikuwa ni wa lazima kwao kutokana na maandalizi ya michuano hiyo waliyoyafanya
kuanzia mwanzo na wamejipanga vizuri katika kuingia katika nusu fainali ya
michuano hiyo na amelaumu kwa wachezaji wake kupewa kadi zisizo za lazima.
‘’Yaa ushindi wa leo ulikua ni wa lazima kwetukutokana na maandalizi
katika mashindano haya tuliyoyafanya tokea mwanzo na tumejipanga vizuri kwa
kufanya mazoezi na leo tumepewa kadi zisizo za lazima ila si kwamba timu haina
nidhamu’’,alisema kocha Kamanda.
 |
Pichani mashabiki wa Sombetini Parish wakisherehekea ushindi dhidi ya Ajtc stars |
Ushindi wa leo umewapa nafasi Sombetini Parish kuwa
na mchezo siku ya ijumaa na wanasema wamejipanga vyema katika kuingia kwenye
mchezo huo na kuahidi ushindi kwa timu hiyo.
Pia IGUNGA NEWS iliweza kuongea na mashabiki wa timu
zote mbili na kusema timu zo zimecheza vilivyo na matokeo yaliyotokea ni moja
ya mchezo na wameahidi kuendelea kuzishabikia timu zao.